MOURINHO NAE AINGIZWA KWENYE ZAHAMA LA KUKWEPA KODI

KOCHA wa sasa wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho nae ametajwa kuwa katika tatizo la kukwepa kodi wakati akiwa kocha wa Real Madrid.

Taarifa iliyotolewa juzi inasema kwamba kocha huyo alifanya udanganyifu akiwa kama kocha wa miamba hao wa Hispania kati ya mwaka 2011 na 2012.

Mourinho anadaiwa kwamba alifanya udanganyifu wa kukwepa kodi inayofikia euro mil 3. 3 wakati huo.

Waendesha mashitaka katika jiji la Madrid wamesema kuwa kocha huyo sasa anaweza kujikuta katika wakati mgumu na huenda akaitwa katika jiji hilo kuyakabili mashitaka yake.

Mourinho anadaiwa akiwa Real Madrid alifanya udanganyifu katika kodi yake inayohusu makazi yake nchini humo.


Anadaiwa kuwa hakuwahi kuweka wazi kima halisi anachopata, jambo ambalo anadaiwa kuwa alifanya kwa masl;ahi yake.

No comments