MSANIII JAGUAR ADAIWA KUANZA "KAMPENI" ZA UBUNGE NCHINI KENYA

KITENDO cha rapa wa Kenya, Jaguar kuanza kutoa misaada kwenye jamii ya wahitaji imetafsiriwa kuwa sehemu ya mkakati wake wa kugombea ubunge, baada ya kutangaza rasmi kuingia kwenye ulingo wa siasa.

Jaguar alitembelea kwenye soko maarufu la Tsunami na kutoa vifaa vya ujenzi ili kukarabati baada ya kuwaka moto.

Staa huyo anatarajia kugombea ubunge katika jimbo Starehe Country kupitia chama cha muungano wa jubilee katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi wa nane mwaka huu.

Jaguar aliposti picha kwenye akaunti yake ya Instagram akiwa anatoa misaada ya vifaa vya ujenzi katika soko hilo na kuandika “kazi imeanza.”


No comments