MSHAMBULIAJI WA RAYON SPORTS YA RWANDA KUTUA SIMBA SC

MSHAMBULIAJI hatari wa Rayon Sports ya Rwanda, Tidiane Kone amelipotiwa kwamba wakati wowote ataanza safari ya kuja Tanzania kufanya mazungumzo na wekundu wa msimbazi, Simba.

Chanzo cha habari kuaminika kinasema kwamba Kone ambaye ni raia wa Ivost Cost anakuja Tanzania kwa mwaliko wa kigogo mmoja wa wekundu hao wa msimbazi.

“Ni kweli anakuja. Tumemfuatilia sana katika Ligi Kuu ya Rwanda, kiwango chake kiko juu sana. Anaweza kuwa msaada mkubwa kama tukielewana,” amesema.

Mchezaji huyo ambaye mashabiki wa soka nchini Rwanda wanamwita “kapatila” kutokana na uwezo wake mkubwa wa kupambana na nguvu kubwa aliyo nayo uwanjani, amekuwa ndiyo mfungaji wa muda wote wa Rayon Sporst.    

No comments