MWANAMUZIKI HALILA TONGOLANGA AFARIKI DUNIA


Mwimbaji aliyefanikiwa kuweka muhuri wake kwenye muziki wa dansi kupitia midundo ya sindimba, Halila Tongolanga (pichani), amefariki dunia baada ya kuugua kwa wiki kadhaa.

Tongalanga amefariki usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa kwa matatizo ya figo.

Mwimbaji huyo aliyetesa na wimbo “Kila Munu Ave na Kwao” alikuwa Muhimbili tangu juzi baada ya kuhamishiwa kutoka kwao Newala.

Mwili wa marehemu Tongolanga ambaye pia alikuwa na soko kubwa nchini Msumbiji, unategemewa kusafirishwa leo kupelekwa kwao Newala kwa mazishi.

No comments