Habari

MZEE AKILIMALI HAAMINI KAMA MANJI AMEJIUZULU KIKWELIKWELI UENYEKITI YANGA

on

YANGA ambao ni watani wa jadi
wa klabu ya Simba, zote za Dar es Salaam wanaopita katika kipindi kigumu tangu
mwenyekiti wao, Yusuph Manji alipotangaza kung’atuka madarakani mwezi uliopita.
Wamekuwa wakishindwa
kutengeneza mambo yao kwa sababu za kiuchumi na walifikia hatua ya kuwataka
wanachama wao waanze kuichangia klabu ili iweze kutimiza malengo yake.

Lakini mtu mmoja mwenye sauti
kubwa katika Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali ni mmoja wa watu ambao alisema wazi
kwamba manji huenda anatikisa kibiriti na hana nia ya kujiuzulu kweli kwani
amekuwa akifanya hivyo na kurejea tena madarakani.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *