MZEE YUSSUF AFIWA NA MKE WAKE MDOGO (CHIKU)


Aliyekuwa mfalme wa taarab Alhaj Mzee Yussuf amefiwa na mke wake wa pili (Chiku).

Chiku amefariki jioni ya leo katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam alipokuwa amepelekwa kujifungua.

Mzee Yussuf ameimbia Saluti5 kuwa alimpeleka mkewe hapo Amana leo saa 10 alasiri kwaajili ya kujifungua na kwa bahati mbaya opereshini (upasuaji) iliyofanywa jioni, haikwenda salama na ikampoteza mkewe na mtoto aliyezaliwa.


Habari zaidi zitakufikia baadae.

No comments