MZIMU WA COSTA BADO WAMTESA CONTE CHELSEA

PAMOJA na kuipa mafanikio makubwa klabu ya Chelsea, ikiwa ni pamoja na kunyakua taji la ubingwa wa Ligi Kuu ya England, kuna wasiwasi kwamba kocha wa kikosi hicho, Antonio Conte anaweza kuondoka.

Baadhi ya mitandao ya kijamii nchini Uingereza imethubutu kuandika kwamba siku za Conte ni kama zinahesabika katika Chelsea baada ya kumshutumu kwamba anaivuruga timu hiyo na hasa baada ya kumuondoa mshambuliaji kipenzi cha wengi, Diego Costa.

Mtanda mmoja umeandika kwamba baada ya kumalizika kwa Ligi mambo yanaonekana sio mazuri kwa kocha huyo kwani watu wake wa karibu wamekuwa wakidai Antonio Conte hana furaha Uingereza hasa kutokana na vyombo vya habari vinavyomwandika kocha huyo.

Wiki za karibuni kocha huyo amekuwa akiandikwa sana katika vichwa vya habari vya magazeti na mitandao mbalimbali baada ya kuibuka kwa tuhuma za kumtumia Diego Costa ujumbe mfupi kwenye simu akimwambia hamtaki.

Inafahamika kwamba tangu Conte akiwa nchini Italia anapenda maisha ya kutotokea sana katika vyombo vya habari, lakini hali inayotokea Uingereza inamsumbua sna kichwa na imekuwa ikimkosesha raha.

Lakini pia taarifa zinadai mmiliki wa klabu ya Chelsea, Roman Abromovich amekuwa tatizo sana na ndio sababu hadi sasa Chelsea hawajasajili kwani tajiri pesa aliyotoa ya usajili ni ndogo kuweza kununua wachezaji wakubwa.

Antonio Conte ana ndoto za kubeba Kombe kubwa la Champions Legue, lakini tayari ameona bajeti ndogo ya usajili inaweza kuwa kikwazo kwake kuchukua Kombe hilo nah ii imemfanya kukosa raha.

Ripoti zimesema Conte sasa amechukia zaidi kwani amekuwa akiandikwa tu kuhusu kununua wachezaji lakini pesa hapewi na sasa anataka kuonana moja kwa moja na Roman Abromovich au Marina Granovaskia ambaye ni kati ya wafanya maamuzi wakuu wa Chelsea.


Conte pia anakosa raha kutokana na kukosa control ya academy ya soka ya Chelsea na mambo yote hayo yanamfanya kuanza kuwaza kuondoka lakini bado kuna nafasi kubwa kubaki kwani Roman anafuatilia kwa karibu kutaka kununua majina makubwa wakiwemo Lukaku na Morata.

No comments