NEMANJA MATIC ATAMANI KUANGUKIA MANCHESTER UNITED MAJIRA YA JOTO

KIUNGO wa Chelsea, Nemanja Matic anataka kujiunga na klabu ya Manchester United majira ya joto, kwa mujibu wa habari.

Matic mwenye umri wa miaka 28, ameanza mechi 30 kwenye kikosi cha kwanza Chelsea kati ya 38 Ligi Kuu Uingereza katika kampeni za 2016/17, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Serbia mkataba wake unafikia kikomo majira ya joto 2019.

Siku za nyuma ilidaiwa kuwa bosi wa Manchester United, Jose Mourinho anatamani sana kuungana tena na Matic Old Trafford na kwa mujibu wa Manchester Evening News, kiungo huyo ameshafanya mazungumzo na meneja wake wa zamani kuhusu uhamisho huo.

Ripoti hizo pia zimedai kuwa Mourinho anaamini kumpata Matic ni kazi rahisi kuliko kumpata Eric Dier wa Tottenham Hotspur na mashetani wekundu watajaribu kuishawishi Chelsea kumwachilia mchezaji huyo wiki chache zijazo.


Mourinho alimrejesha Matic Chelsea Januari 2014, miaka mitatu baada ya kiungo huyo kuuzwa Benfica.

No comments