NEMANJA MATIC KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED MAJIRA YA JOTO

KIUNGO wa Chelsea, Nemanja Matic anataka kujiunga na klabu ya Manchester United majira ya joto kwa mujibu wa habari.

Matic mwenye umri wa miaka 28, ameanza mechi 30 kikosi cha kwanza Chelsea kati ya 38 Ligi kuu Uingereza katika kampeni za 2016-17, lakini mchezaji huyo wa kimataija wa Serbia mkataba wake unafikia kikomo majira ya joto 2019.

Siku za nyuma ilidaiwa kuwa bosi wa Manchester United Jose Mourinho anatamani sana kuungana tena na Matic Old Trafford, na kwa mujibu wa Manchester Evening News kiungo huyo ameshafanya mazungumzo na meneja wake wa zamani kuhusu uhamisho huo.

Ripoti hizo pia zimedai kuwa Mourinho anaamini kumpata Matic ni kazi rahisI kuliko kumpata Eric Dier wa Tottenham Hotspur na mashetani wekundu wataijaribu kuishawishi Chelsea kumwachia mchezaji huyo wiki chache zijazo.


Mourinho alimrejesha Matic Chelsea Januari 2014, miaka mitatu baada ya kiumbe huyo kuuzwa Benfica.

No comments