NEW AUDIO: BAADA YA UKIMYA WA MUDA MREFU, H MBIZO AIBUKA UPYA NA WIMBO "MATANGO NYANYA"

Staa wa wimbo mkali wa “Mchumba” au Nilonge nisilonge kama ulivyokuwa ukifahamika na wengi, H Mbizo, ameibuka na wimbo mpya “Matango Nyanya”.

H Mbizo ambaye amekuwa kimya kwa miaka mingi, ameachia ngoma hiyo kupitia mkono wa producer Mo Fire.

Kwa muda mrefu H Mbizo alikuwa akijishughulisha kuwaandikia wasanii nyimbo, ikiwemo “Majanga” ya Snura, lakini sasa ameamua kurudi kwenye game kupitia “Matango Nyanya”.

No comments