NEW AUDIO: MAPACHA BAND YACHOMOA MAKUCHA KUPITIA “DUNIA SIMAMA” …Jose Mara bado yuko imara
Mapacha Band imeshuka na kazi yake ya kwanza kabisa tangu kukarabatiwa jina kutoka Mapacha Watatu.

Nyimbo inakwenda kwa jina la “Dunia Simama” utunzi wake bosi wa bendi Jose Mara ambaye anaonyesha kuwa yupo imara hata baada ya wakurugenzi wenzake Kalala Jr na Khalid Chokoraa ‘kujitosa bahari’ mmoja baada ya mwingine.

Ni nyimbo yenye madongo kwa mwenye sikio la udadisi na kwa mwenye akili ya utambuzi.

Ama kwa hakika ni kazi nzuri inayoashiria mema katika ujio mpya wa Mapacha. Isikilize hapo juu.

No comments