NEW AUDIO: “RAFIKI SHILAWADU” KUTOKA KWA JIMMY MANZAKA AKIMSHIRIKISHA BUSHOKEJimmy Manzaka ni mwimbaji aliyetamba na bendi ya Rufita Connection miaka kadhaa iliyopita akiwa sambamba na marehemu Banza Stone.

Kwasasa anaishi Dubai akimiliki bendi yake lakini kwa muda huu akiwa mapumzikoni hapa Tanzania, anaachia ngoma kali inayokwenda kwa jina la “Rafiki Shilawadu”.

Kazi hii imepakuliwa katika studio za Soft Records chini ya producer Pitchou Mechant ambapo ndani yake Jimmy Manzaka amemshirikisha nyota wa muziki wa kizazi kipya Bushoke.

Isikilize kazi hii mpya ya Jimmy Manzaka ambaye ni mjomba wake na rais wa FM Academia Nyoshi el Saadat.

No comments