NEYMAR AJIANDAA KUWAACHA “PACHA” WAKE MESSI NA SUAREZ… yadaiwa kujiandaa kutua Real Madrid

INAWEZA kuwa ni habari mbaya kwa wapenzi wa FC Barcelona duniani kote.

Habari yenyewe ni kwamba mwanasoka mwenye mvuto kuliko wote katika kikosi chao, Neymar Jr anajiandaa kuhamia kwa mahasimu wao wakubwa, Real Madrid.

Gazeti moja nchini Hispania limeandika kwamba mwanasoka huyo raia wa Brazil anakamilisha mipango ya kuhamia Real Madrid kutokana na kuchoshwa na mambo yanavyokwenda katika kikosi cha Barcelona.

“Neymar kuna wakati alikuwa ahamie kwetu, lakini mambo hayakuwa kama tulivyotaka. Lakini sasa tunamtaka tena,” amesema rais wa Real Madrid, Florentino Perez.

Hata hivyo, amesema kwamba sasa anaona kwamba kuna nafasi ya kumvuta tena kwao.

“Anaweza kuhamia Real Madrid na wakati mwafaka utafika. Sina hakika kama kuna makubaliano yoyote kati yake na klabu yake,” limeandika gazeti hilo.

Perez amesema itakuwa jambo la maana kabisa kama mwanasoka huyo nyota atahamia kwenye kikosi chao.

Mwanasoka huyo wa Brazil alijiunga na Barcelona mwaka 2013 na alitengeneza pacha kubwa kati yake na washambuliaji wawili; Lionel Messi na Luis Suarez.

Hata hivyo, imedaiwa kuwa mwanasoka huyo atahamia Real Madrid kama cristiano Ronaldo ataondoka kwenye kikosi hicho.

Ronaldo amekuwa akihusishwa na kuondoka katika kikosi hicho kufuatia kili alichosema kwamba hajapewa ushirikiano na klabu hiyo katika madhira ya kodi yanayomhusu.


“Neymar alifaulu mpaka vipimo vya afya katika Madrid. Tulijaribu kumleta hapa wakati fulani lakini tukaachana na ile mipango,” alisema Perez akiongea na radio moja ya nchini Hispania, Onda Cero.

No comments