NGOMA AWAZODOA WANAOPAKAZA KUWA NJIANI KUTUA SIMBA

SIMBA imepewa taarifa mbaya na mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma akiwaambia hajafanya maamuzi ya kuondoka Yanga na kwamba safari yake ya kuja nchini ni kumalizana na klabu yake hiyo.

Akiongea na saluti5 kutoka kwao Zimbabwe, Ngoma amesema anasikia taarifa za yeye kusubiriwa kusaini Simba lakini hakuna lolote mpaka sasa alilolifanya na klabu hiyo na anachojua ni ofa ya Yanga.

Ngoma alisema, bado ana imani na Yanga na kwamba kwa sasa yuko katika mazungumzo na viongozi wa Yanga ambao ndio waliomtumia tiketi ya kumrejesha nchini na sio Simba.

Mshambuliaji huyo alisema bado hajafikiria kucheza klabu yoyote nchini tofauti na Yanga na kwamba endapo itatokea akashindana na Yanga atarudi kwao Zimbabwe na kuendelea na FC Platnum ambayo bado inamuhitaji.

“Kuna mambo mengi Tanzania yanazungumzwa eti mimi nataka kwenda Simba, hakuna kiongozi wa Simba aliyeongea na mimi. Waliwahi kunifuata lakini nikawapa msimamo wangu kwamba bado niko Yanga,” alisema Ngoma.


“Kwa sasa mashabiki wa Yanga wanatakiwa kutambua niko katika mazungumzo na Yanga na sio Simba, hata tiketi yangu ya kuja huko nimetumiwa na Yanga, sasa utaona kwamba hizo taarifa sio sahihi.”

No comments