Habari

NGOMA, KAMUSOKO WATULIZA PRESHA JANGWANI

on

KIUNGO Thaban Kamusoko na mshambuliaji
Donald Ngoma wametuliza mzuka baada ya kuwaambia mabosi wa Yanga kwamba wapo
tayari kubaki kwa muda zaidi katika kikosi hicho.
Taarifa zilizoifikia saluti5
zimesemsema Kamusoko amesema anakuja nchini wiki hii kumalizana na Yanga baada
ya mafanikio katika mazungumzo ya kuongeza mkataba zaidi.
Kiungo huyo fundi amesema
anataka kubaki Yanga ambayo imempa heshima kubwa hasa baada ya hivi karibuni kurejeshwa
katika kikosi cha taifa na kwamba haoni kama watashindwa katika mazungumzo ya
mwisho yatakayofanyika hapa nchini mara baada ya kuwasili.
“Nitakuja hapo Tanzania wiki
hii, nimeshazungumza na viongozi na tuko katika sehemu nzuri. Wana Yanga wasiwe
na wasiwasi, hakuna kitakachoshindikana,” alisema Kamusoko.
Wakati Kamusoko akiyasema hayo,
mmoja wa mabosi wa usajili, amesema Ngoma amekubali kusaini mkataba mpya wa
kubaki ambapo hatma yake nae itajulikana mara baada ya kuwasili.

Ngoma ambaye kwa sasa yuko kwao
Zimbabwe kwa mapumziko, inaelezwa kiasi cha dola 40,000 kitatumika katika
kumuongezea mkataba huo ambapo utakuwa mkataba wa pili kwake na Yanga.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *