NOVAK DJOKOVIC ASEMA "SIO MBAYA" MAISHA YA MICHEZO BILA MWALIMU WAKE

MKALI anayeshika nafasi ya nne katika viwango vya ubora katika mchezo wa tenisi kwa upande wa wanaume, Novak Djokovic amesema hana jinsi amekubaliana na maamuzi ya mwalimu wake, Boris Becker.

“Ni salama kutokuwa na kocha?” aliulizwa mkali huyo.

“Nafurahia safari hii, najisikia ni kama naanza kitu upya, napenmda sana changamoto, mimi ni mwindaji na hakuna furaha kama kupata ushindi ukiwa umetoka jasho ukiwa peke yako,” alisema Djokovic alipokuwa akifanyiwa mahojiano na kituo kimoja cha michezo nchini Serbia.

Mwezi mmoja baada ya kuondoka kwa mwalimu wake, tayari mkali huyo ameanza kupoteza katika mchezo huo kwani tayari amepoteza mapambano manne dhidi ya Denis Istomin katika mashindano Australia Open, lakini pia mbele ya Martin Klizan katika mashindano ya Mexican Open.


Mengine mawili amepoteza mbele ya Nick Kyrgios katika michuano ya Indian Wells pamoja na mashindano ya Monte Carlo Masters Rolex aliyopoteza mbele ya Mbelgiji David Goffin.

No comments