NYOTA WA SEVILLA AKIRI KUWA NA MAHABA NDANI YA CHELSEA

NYOTA wa klabu ya Sevilla anayecheza kwa mkopo katika kikosi cha Atletico Madrid, Matias Kranevitter amekiri mapenzi aliyonayo ya kuona siku moja anaichezea timu ya Chelsea.

Awali, Kranevitter amekuwa akihusishwa na tetesi za kujiunga kwa washika mitutu wa jiji la London na Arsene Wenger ameweka mezani ofa kwa ajili yake.

Lakini kocha wa sasa, Antonio Conte inasemekana ameingilia kati dili hilo na anapambana kuhakikisha kiungo huyo anatua katika kikosi cha Stanford Bridge katika usajili wa dirisha la majira ya joto.

“Nimekuwa nikisikia malengo ya Conte kwangu  na kadri ninavyotambua mpango uko hivyo, nami binafsi napenda kucheza katika kikosi cha Chelsea.”

“Ni kati ya makocha wazuri duniani wanaovutia kufanya kazi nao. Kila mchezaji anaota ndoto ya kufundishwa na mwalimu wa mfano wake.”

“Kwa nyakati tofauti nimekuwa nikifundishwa na makocha wengine. Kama kuna siku inatokea Napata nafasi ya kufanya kazi chini yake nitakuwa na furaha kubwa.”


“Lakini kwa sasa bado niko Atletico kwa mkopo. Najisikia furaha kuwa hapa. Hakuna tatizo kuwa hapa,” alisisitiza Matias Kranevitter.

No comments