OKWI AWAHAKIKISHIA FURAHA WANA MSIMBAZI

BAADA ya Jumatano hii kufuata mabegi nyumbani kwao Kampala Uganda kufuatia kumwaga wino wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Simba, kiungo mshambuliaji, Emmanuel Okwi.

Okwi ambaye ni kipenzi cha mashabiki wengi wa Simba kutokana na kazi nzuri aliowafanyia wekundu hao miaka ya nyuma, alisema anajua mashabiki wa klabu hiyo wana kiu na mafanikio ambayo wameyakosa kwa miaka minne.

“Nashukuru viongozi wa Simba kunikaribisha tena, tumekuja kufanya kazi na viongozi ambao wana njaa ya kupata mafanikio, nimekuja kupambana kuhakikisha tunachukua ubingwa msimu ujao na kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.”

“Pia namshukuru sana Mohammed Dewji “Mo” kwa kufanikisha uhamisho wangu na kurudi tena Simba kwa mara nyingine,” alisema Okwi.

Alisema, Simba ni timu yake, imemsaidia katika mafanikio yake kwa hiyo kurudi kwake ni kama amerudi nyumbani na wana imani nae, hivyo hatawaangusha, atajituma kwa ajili ya kuipigania Simba.

Kurejea kwa straika huyo kumerejesha furaha ya mashabiki wa wekundu hao wa Msimbazi wakiamini tatizo lao la safu ya ushambuliaji la kupachika mabao mengi limeshazingatiwa pia kwamba yupo John Bocco ambae alisajiliwa kutoka Azam FC.

Okwi anajiunga na Simba akitokea SC Villa ya nchini kwao Uganda ambayo nayo ilimpokea akitokea kukipiga na timu ya SonderjyskE ya nchini Demark ambayo alivunja nayo mkataba baada ya kuchoshwa na kusuguliwa benchi.

Simba inakabiliwa na michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani, ndio maana wanafanya usajili wa nguvu ikizingatiwa wana misimu mingi bila kushiriki michuano hiyo.

No comments