OMONI OBOLI WA NOLLYWOOD ATANGAZA MPANGO WA KUACHIA FILAMU YA KOMEDI

OMONI Oboli ambaye ni staa wa Nollywood ametangaza mpango wake wa kuachia filamu ya vichekesho huku ikiwa na maudhui ya mapenzi, aliyoipa jina la “Okafor’s Law”.

Filamu hiyo itajumuisha mastaa wenye majina makubwa kama Richard Mofe Damijo, Blossom Chukwujekwu, Ufuoma McDermott, Kemi Lala Akindoju, Yvonne Jegede, Halima Abubakar na Mary Lazarus.

Okafor’s Law ambaye alihudhuria tamasha la filamu nchini Canada katika jiji la Toronto, amesema kuwa kwa hivi sasa atajikita zaidi kwenye sanaa za vichekesho.

“Mpango wangu ni kuzidi kucheza filamu za Komedi kwa sababu nahisi nina kipaji katika ulingo huo, nataka kuonyesha uwezo kwenye ulingo huu,” alisema staa huyo.

No comments