OXLADE-CHAMBERLAIN AMWAMBIA WENGER ‘KAZA BUTI USAJLI MASTAA’


STAA wa Arsenal, Alex Oxlade-Chamberlain, amemchagiza kocha wake Arsene Wenger kuhakikisha anafanikiwa kuwasajili washambuliaji Kylian Mbappe wa Monaco na Alexandre Lacazette wa Lyon kiangazi hiki licha ya kuwa atalazimika kutumia fedha nyingi.

Baada ya kujaribu na kushindwa kumsainisha Mbappe mwaka jana, Wenger amerejea tena katika mbio za kuwania saini ya straika huyo kinda, lakini akikabiliwa na ushindani kutoka Real Madrid, Chelsea, Manchester City na Paris Saint-Germain.

Lacazette pia alifukuziwa na Wenger kiangazi kilichopita, lakini ofa yake ya pauni milioni 29 ilikataliwa na Lyon.

Kiangazi hiki, bei ya staa huyo wa kimataifa wa Ufaransa imefika pauni milioni 60 na inawezekana uhamisho wa Mbappe ukagharimu zaidi ya pauni milioni 100.

“Kila mmoja anawataka katika timu yao,” alisema Oxlade-Chamberlain akizungumza na gazeti la Evening Standard.

No comments