PAUL KIONGERA ALIYETEMWA KWA KIWANGO KIBOVU SIMBA ATUA TENA DAR ES SALAAM

SIMBA iliachana na straika ambaye alikuwa anatarajia kuonyesha makali yake kwa kiwango kikubwa, Paul Raphael Kiongera lakini mchezaji huyo akateswa na majeruhi, ajabu ni kwamba Kiongera akiwa nchini kwake Kenya anacheza kwa kiwango cha juu lakini akija Tanzania mambo yanakuwa mabaya.

Kiongera sasa anacheza kwenye kikosi cha AFC Leopards ya Kenya na anatarajiwa kuonyesha tena cheche zake katika michuano ya Sportpesa Super Cup iliyoanza wiki hii.

Paul Raphael Kiongera ni mmoja wa wachezaji wa AFC Leopards wanaotarajiwa kuwa chini ya kocha wa zamani wa Ndanda FC na Azam, raia wa Tanzania, Dennis Kitambi.

Klabu ya AFC Leopards ya nchini Kenya tayari imetangaza kikosi chake cha wachezaji 20 kwa ajili ya Kombe la Sportpesa.

Mshambuliaji huyo wa Simba ataongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo. Washambuliaji wengine ni Mghana Gilbert Fiamenyo na Mganda Alan Katelega.


Kitambi amekabidhiwa jukumu la kuinoa AFC Leopards katika michuano ya Sportspesa kufuatia kubwaga manyanga kwa kocha Stewart Hall.

No comments