"PEP GUARDIOLA ANANITAKA LEO KESHO" PASTORE WA PSG APASUA

NYOTA wa klabu ya PSG, Javier Pastore amekiri kuwindwa na kocha wa sasa wa Manchester City, Pep Guardiola kwani mpango huo umeshindwa pia kukamilika katika usajili wa mwezi Januari, mwaka jana.

Kocha Pep aliweka jina la Javier Pastore katika orodha yake ya wachezaji anaowawania.

Akinukuliwa, Pastore amesema ndoto za Guardiola ziliyeyuka baada ya PSG kutaka ofa ya kuuzwa kwake.

“Ninakiri kusema kuwa Man City imekuwa ikiniwinda kwa vipindi tofauti, lakini dili limekuwa likikwama.”

“Hata katika usajili wa dirisha la januari nilikuwa na mazungumzo nao lakini haikuwezekana kwani bado nipo na nina matarajio makubwa hapa.”

“Bado nipo PSG. Ninajisiki furh kuwa hapa, hakuna tatizo kuwa hapa.”

“Kucheza katika timu inayoshiriki Ligi y Mabingw ni kati ya malengo yangu, pia kila mchezaji anaota mafanikio kama hayo.”


“Ninataraji kuwa katika kiwango hicho cha mafanikio, ninaamini kuwa siku nitafikia hatua hiyo, ni suala tu la kusubiri kuona,” alisisitiza Pastore.

No comments