PEP GUARDIOLA APIGA HESABU ZA KUMSAJILI INIESTA MAN CITY


LISEMWALO lipo na kama halipo lipo njiani laja. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema wakati kukiwa na taarifa katika baadhi ya magazeti na mitandao ya jamii kwamba Pep Guardiola anajaribu kumshawishi Andres Iniesta kujiunga naye Manchester City.

Kiungo huyo mkongwe raia wa Hispania, alikuwa na uhusiano mzuri na Guardiola wakati wakiwa wote Barcelona na sasa wanaweza kuwa karibu tena Manchester City.

Mtandao wa Calciomercato wa Italia umeripoti kwamba Guardiola ana nia ya kufanya kazi tena sambamba na kiungo huyo ambaye amebakisha mwaka mmoja Barcelona na bado hajakubali kusaini mkataba mpya.

Calciomercato imeripoti kwamba Guardiola amewasiliana na kiungo huyo wa miaka 33 na kumshawishi kuungana naye Etihad, ambako anaweza kupata tena mafanikio sawa na aliyopata Nou Camp.

Guardiola na Iniesta walishinda mataji matatu ya La Liga na mawili ya Ulaya katika kipindi cha miaka minne walichokuwa pamoja Nou Camp.

No comments