Habari

PICHA 23 ZA MAZISHI YA MWIMBAJI MKONGWE AHMAD MANYEMA

on

MAMIA ya wanamuziki, mashabiki na wadau mbalimbali walikusanyika kwa
wingi Jumatatu mchana katika maziko ya mkongwe wa miondoko ya dansi nchini,
Ahmad Majuto Goba maarufu kama “Ahmad Manyema”.
Manyema amefariki dunia Jumamosi majira ya saa 3 za usiku hospitali ya
Mwananyamala, jijini Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi
ya moyo, pumu, miguu na kutapika damu.
Manyema ambaye wakati wa uhai wake alitamba zaidi na bendi za Dar
Jazz, Kilwa Jazz, JKT, Tanga International, Les Mwenge na Santon Sound,
amezikwa saa 7:00 mchana, kwenye makaburi ya Mwembe Tango, Mabibo, Dar es
Salaam.
Marehemu ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 65, ambapo ameacha mke na
watoto wanne ambao ni Majuto, Shaaban, Leylat na Hassan.
 Waimbaji wa Mlimani Park Sikinde, Abdallah Hemba (kushoto), akiwa na mwimbaji mwenzie wa Vijana Jazz, Abdallah Mgonahazeru nyumbani kwa marehemu Ahemed Manyema 
 Baadhi ya wanakuziki na wadau wa dansi wakisubiri taratibu za maziko ya Manyema zianze kuelekea makaburini
 Michango ya hapa na pale ilikuwa ikiendelea katika kufanikisha shughuli ya maziko
 Hapa ni baadhi ya akinamama ambao ni wanafamilia
 Wanamuziki na waandishi wa habari katika picha ya pamoja eneo la tukio
 Wasanii wakiendelea kusubiri kuanza kwa msafara wa mazishi kuelekea makaburini
 Wanamuziki wakibadilishana mawili matatu
 Watangazaji Mwinyi Ami wa Magic Fm pamoja na Rajab Zomboko wa Radio One na ITV katika picha ya pamoja na mmoja wa wadau wa dansi, Babu Onesmo “Mzee wa Madikodiko”
 Hapa ibada ya kuswalia wili wa marehemu imeanza
 Ibada inaendelea
 Mwenyekiti wa CHAMUDATA, Juma Ubao akikabidhi mchango wa chama hicho kwa mtoto wa marehemu, Majuto Ahmad
 Mmoja wa watto wa marehemu, Hassan (aliyevaa jinzi na fulana), akifuatilia ibada ya kuswalia mwili wa marehemu baba yake 
 Waumini katikati ya ibada
 Kijana Majuto akionyesha kushindwa kuhimili simanzi na huzuni ya kif cha baba yake na kuanza kuangua kilio kikubwa
 Kutoka kushoto, Hemba, Mwimjuma Muumin na Zomboko wakiitikia dua kabla ya safari ya kuelekea makaburini
 Hapa sala ya mwili wa marehemu inahitimishwa rasmi
 Safari kuelekea makaburini ikaanza 
 Sehemu ya umati mkubwa wa watu wakisubiri kupokea jeneza kuelekea makaburini
 Mpuliza Tarubeta wa Sikinde, Mbaraka Othman akipokea jeneza kuashiria kumuaga mwanamuziki mwemzake 
 Mwili wa marehemu Manyema ukiwasili akaburini
 Maziko yanaendelea
 Shughuli ya mazishi ikiwa katika hatua za mwisho
 Wanamuziki George Gama (kushoto) na mcharaza Drums mahiri, Mwampashi
Hapa kaburi la marehemu Manyema likimaliziwa kufukiwa 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *