Habari

PICHA 25 ZA MAZISHI YA MKE WA MZEE YUSSUF

on

Mamia ya watu wakiwemo wadau na wasanii mbali mbali wa muziki,
walitijitokeza makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam kumzika Chiku – mke mdogo wa
Mzee Yussuf.
Mazishi hayo yalifanyika saa 7.30 mchana ambapo mtoto mchanga wa
marehemu, alizikwa kando ya kaburi la mama yake.
Ilikuwa ni simanzi kubwa kwa Mzee Yussuf ambaye licha ya kujitahidi
kuwa mkakamavu katika muda wote, lakini mambo yalimwia vigumu baada ya mazishi
na ikabidi apate msaada wa kushikwa huku na huku wakati wa kuondoka makaburini.
Chiku alifariki Jumamosi jioni katika hospitali ya Amana, Ilala kwa
matatizo ya uzazi uliompoteza yeye na mtoto wa kiume aliyezaliwa.
 Safari ya kuelekea makaburini inaanza
 Kuelekea makaburi ya Kisutu
 Mfanyabiashara Eric Shigongo (mwenye shati la kitenge) akiwa makaburini muda mfupi kabla mwili haujawasili
 Kaburi la mama na mwanae
 Mzee Yussuf akikumbatia mwili wa mwanae
 Maandalizi ya kuhifadhi mwili yakiendelea
 Mzee Yussuf akiupokea mwili wa mkewe
 Mazishi yanaendelea
 Mwili wa mtoto nao unaingizwa makaburini
 Mazishi yanaendelea
 Harakati za mazishi zikiendelea
 Taswira ya mazishi ya mke wa Mzee Yussuf
 Mzee Yussuf akiweka mchanga kwenye kaburi la mkewe
 Mazishi yanaendelea
 Baadhi ya wadau wa muziki wakiwa makaburini
 Umati wa watu uliofurika makaburini
 Mashallah! ama kwa hakika mazishi yalikuwa makubwa
 Wakati wa kisomo
 Mzee Yussuf kwenye hisia nzito
 Wadau wa muziki
 Mzee Yussuf akiwa na ndugu na jamaa kwenye kaburi la mkewe
 Mzee Yussuf akiondoka makaburini huku akiwa taaban
Hali ilikuwa tete kwa Mzee Yussuf wakati wa kuondoka

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *