PIUS BUSWITA AZICHANGANYA SIMBA NA YANGA... sasa ni mali ya Jangwani

HABARI zilizotingisha duru za michezo Ijumaa mchana ni zile za kiungo wa Mbao FC, Pius Buswita kumwaga wino katika klabu ya Yanga.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa Simba imejiingiza katika utata wa kumsajili Buswita aliyetangulia kusaini Yanga na ikasemekana kuwa hatua hiyo ingemuingiza katika uwezekano wa kufungiwa.

Kwa sasa Buswita ni mchezaji wa Yanga baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili huku Simba wakiwa wamebaki wanashangaa.

Simba katika ushawishi wao wakati wanamwania kiungo huyo, walitangulia kumshawishi kaka wa Buswita ambaye alikubali kisha kumbadilisha akili nduguye na baadae kudaiwa kusaini mkataba na wekundu hao wa Msimbazi.


Inasem,ekana Simba walishakubaliana kila kitu na mchezaji huyo na kubaki suala la kusaini tu ambapo fedha ikawa kikwazo na Yanga wakatumia nafasi hiyo kuwapindua na kuwazidi kete.

No comments