Habari

Q CHILLAH AMWAGA CHOZI KUMLILIA “CHID BENZ”

on

STAA wa muziki wa kizazi kipya,
Q Chillah ametambulisha wimbo mpya  alioshirikishwa
na rapa Chid Benz kwa staili  ya  kumwaga machozi wakati akiwa kwenye  mahojiano.

Q Chillah alisema kwamba anaguswa
na hali ya Chid Benz ambaye alikaa kwenye 
rehab kwa muda mrefu akitibu tatito la matumizi ya dawa  za kulevya.
“Nimeguswa na hali ya Chid Benz
na najua nimepitia  hali nyingi sana kwenye
maisha ambazo Chid pia amepita,” alisema rapa huyo .
“Lakini kikubwa kilichoniliza
nimewahi kuwapoteza marafiki wakubwa sana ambao niliwapenda, wasanii wenye majina
makubwa Tanzania, mtu kama Albert Mangweha “Ngawair” Mwana hiphop ambaye mimi
sijawahi kumuona zaidi yake,” alimaliza rapa huyo.

Marapa hao Q Chillah na Chid Benz
kwa wakati tofauti wote waliwahi kukiri kuathiriwa na matumizi ya dawa za kulevya.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *