RAMA PENTAGONE ASEMA MWEZI WA RAMADHANI UNAMTOA "SHAVU DODO"

MWIMBAJI na mmoja wa viongozi waandamizi wa Ivory Band, rama Pentagone amesema anajiona kuwa na amani zaidi katika kipindi hiki mwezi mtukufu wa ramadhani ambapo anaungana na waumini wenzake wa dini ya Kiislamuu duniani kutekeleza ibada ya swaumu.

Akiongea na saluti5, Pentagone amesema kuwa, anahisi hata nuru ya sura na mwili wake imekuwa ni inayong’aa zaidi, huku akieleza kwamba mfungo huu mtukufu umemfanya awe “shavu dodo”.

“Nawasisitiza ndugu zangu waislamu wote tujitahidi zaidi kumcha Mungu wetu kwa kipindi hiki na kuachana na yale yote ambayo yanaweza kututia majaribuni, mwezi mmoja si kitu kwa mwaka mzima tunashindwa nini,” amesema Pentagone.


Aidha, pentagone amewataka waislamu wenzake kuacha kusingizia magonjwa ili kupata sababu ya kukosa kushiriki ibada hiyo ya swaumu, kama ambavyo baadhi yao wamekuwa wakidai wana vidonda vya tumbo kila inapofikia kipindi hiki.

No comments