RAMADHANI REDONDO ASUBIRI TIMU MWAFAKA KUJIUNGA NAYO

ALIYEKUWA kiungo wa Mbeya City, Ramadhani Chombo “Redondo” amesema kuwa hivi sasa yuko huru akisubiri timu inayoeleweka ili aweze kujiunga nayo msimu ujao.
Kiungo huyo ambaye aliwahi kutiomkia Denmark wakati akiwa kwenye kituo cha Dyoc, amesema kuwa kuna timu zinamnyemelea lakini bado hawajafikia makubaliano.
“Nipo huru hivi sasa, bado hakuna timu tuliyofikia makubaliano kwa ajili ya msimu ujao. Nasubiri kuona nini kitaendelea,” alisema Redondo.
“Nipo kwenye mapumziko ya muda mfupi kabla ya kujua wapi nitaelekea msimu ujao, nitaweka wazi nikishafikai makubaliano na sehemu nitakayoenda,” alimaliza.
Ramadhani Redondo aliwahi kuitumikia klabu ya Simba kabla ya kutimkia Mbeya City.

No comments