REAL MADRID YAIPA 'ZA USO' MANCHESTER UNITED KWA MORATA


MANCHESTER UNITED wameambiwa kuwa wanahitajika kuongeza ofa yao kwa Alvaro Morata baada ya mazunguzo na Real Madrid yaliyoshindwa kuzaa matunda Jumatano.

Kwa mujibu wa redio ya mtandaoni ya COPE, wakala wa straika huyo Mhispania, Juanma Lopez, alikutana na maofisa wa Real Bernabeu akiiwakilisha United kuwafahamisha uamuzi wa Morata kuondoka na kuweka dili mezani.

Hata hivyo dau la awali la United – pauni milioni 52.4 lilikataliwa na kwamba Real wanataka karibu pauni milioni 65.

Gazeti la AS limeripoti kuwa Morata anataka dili kukamilika haraka kabla kufunga ndoa na mchumba wake Alice Campello mjini Venice Ijumaa.

Kwa mujibu wa gazeti la Mirror, straika huyo ataungana tena na Jose Mourinho "mapema wiki ijayo ", kwamba vipimo vya afya vinaweza kufanyika wikiendi hii na dili kutangazwa kukamilika Jumatatu.

No comments