REAL MADRID YAONGOZA MBIO ZA KUSAKA SAINI YA KYLIAN MBAPPEREAL MADRID imeripotiwa kuwa na matumaini ya kunasa saini ya mshambuliaji kinda wa Monaco, Kylian Mbappe kwa dau la pauni milioni 100 na kisha kumwacha katika klabu hiyo ya Ligue 1 kwa mkopo wa mwaka mmoja.

Kwa mujibu wa gazeti la AS, Los Blancos inaamini kuwa ofa hiyo ni kishawishi tosha kwa Monaco na uchawi tosha dhidi ya Paris Saint-Germain ambayo pia inatajwa kumfukuzia straika huyo wa miaka 18 aliyemaliza msimu na mabao 26, huku ‘akipika’ mengine 14 kwa wenzake na kuisaidia klabu yake kuibuka na ubingwa wa Ligue 1.

Awali inaelezwa kuwa Monaco ilikataa ofa ya pauni milioni 103 kutoka Real, ambayo hata hivyo haikuwa imejumuisha kipengele cha kumwacha kinda huyo Mfaransa aendelee kucheza Ligue 1 kwa msimu mmoja.


Kwa mujibu wa mwandishi Matt Spiro wa Le Parisien, Monaco imemuweka kinda huyo katika mipango yake kiangazi hiki na inajaribu kumshawishi abaki.

No comments