REAL MADRID YASEMA "LETENI EURO MIL 180 MUMCHUKUE RONALDO"

BAADA ya kubeba Kombe la Ligi Kuu Hispania na michuano ya Klabu Bingwa Ulaya, Real Madrid imesema iko tayari kupokea ofa ya euro mil 180 kwa ajili ya Cristiano Ronaldo.

Klabu nyingi zinaitaka saini ya mshindi huyo wa tuzo ya Ballon d’Or mara nne na zinaweza kujaribu kumnasa.


Klabu za Manchester United, PSG na Monaco zinapigana vikumbo kumpata, lakini pia kuna ofa kutoka klabu za China.

No comments