REAL MADRID YATWAA UBINGWA ULAYA KIULANI, JUVE YAKUBALI 4-1 …Ronaldo moto chini


Real Madrid wametwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuinyuka Juventus 4-1 kwenye mchezo wa upande mmoja wa fainali.

Mchezaji bora wa dunia, Cristiano Ronaldo ndiye aliyekuwa mwiba kwa Juventus kwa kutumbukiza wavuni mabao mawili na kuifanya Real Madrid iwe timu ya kwanza kufanikiwa kutetena taji.

Ronaldo alifunga bao la kwanza dakika ya dakika ya 20 lakini Mario Mandzukic akachomoa dakika ya 27 na kulazimisha timu hizo kwenda mapumziko zikiwa nguvu sawa.

Udhaifu wa Juventus ulionekana wazi katika kipindi cha pili ambacho iliruhusu mpira kuchezwa kwenye nusu yao kwa muda wote.


Real Madrid wakiwa wanamiliki mpira watakavyo, wakapata bao la pili dakika ya 61 kupitia shuti la mbali la Casemiro kabla Ronaldo hajafunga goli la tatu dakika ya tatu baadae kufuatia pasi tamu ya Modrick huku Marco Asensio akitupia la nne kunako dakika ya 90.

Juventus (4-2-3-1): Buffon, Alves, Barzagli (Cuadrado 66), Bonucci, Chiellini, Sandro, Pjanic (Marchisio 70), Khedira, Higuain, Dybala (Lemina 78), Mandzukic

Real Madrid (4-3-1-2): Navas, Carvajal, Ramos, Varane, Marcelo, Kroos (Morata 89), Casemiro, Modric, Isco (Asensio 82), Benzema (Bale 77), Ronaldo

No comments