REAL SOCIEDAD YAMWINDA ADNAN JANUZAJ

KINDA wa klabu ya Manchester United, Adnan Januzaj ameripotiwa kuwa kwenye rada za Real Sociedad ya nchini Hispania.

Rais wa klabu hiyo, Jokin Aperribay amethibitisha taarifa za kumuwania kinda huyo ambaye hatima yake Old Trafford bado iko shakani.


Januzaj alikuwa na mwanzo mzuri katika kikosi cha Man United kabla mambo hayajaanza kumwendea kombo na kutolewa kwa mkopo wa muda mrefu.

No comments