Habari

RENATO SANCHEZ WA BAYERN MUNICH ANUKIA MANCHESTER UNITED …Douglas Costa naye awekwa sokoni

on

Bayern Munich ipo tayari kuwapiga bei Douglas Costa na Renato Sanches iwapo pesa sahihi itawekwa mezani, hatua itakayopokewa vizuri na Manchester United.
Gazeti la Bild la Ujerumani limedai kocha Carlo Ancelotti anataka kusajili wakali wapya Bayern Munich na njia pekee ni kuwaweka sokoni  Costa na Sanches. 
Mabingwa hao wa Ujerumani wanataka angalau pauni milioni 6o kwa nyota hao wawili ambao waliwahi kuwaniwa na Manchester United na Tottenham.
United ilikaribia kumsajili Sanches kiangazi kilichopita kabla hajaamua kwenda Bayern Munich kwa pauni milioni 28 ambazo zinaweza kuongezeka hadi pauni milioni 60 iwapo kinda huyo wa miaka 19 atang’ara kwenye klabu yake na kwa timu ya taifa ya Ureno.
Inaaminika pia kuwa Bayern inataka kumuuza Sanches kabla bei yake haijapanda kufikia pauni milioni 6o.
Mourinho alikiri kuwa alitaka kumsajili kiungo huyo kutoka Benfica ya Ureno lakini alichelewa. “Nilichelewa kuwasili Manchester United, nilisaini mwezi Mei, kama ningefika mapema ningempigania,” alisema Mourinho.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *