RIPOTI YA RWANDAMINA YAMWITAJI NGOMA KIKOSINI

RIPOTI ya kocha mkuu wa Yanga, George Rwandamina imebainisha kuwa bado anamwitaji mshambuliaji wake nyota, Donald Ngoma na kwamba yuko kwenye mipango yake ya baadae ya kikosi hicho.

Licha ya Ngoma kutoshuka dimbani kwa muda mrefu kutokana na majeruhi, lakini Lwandamina amebainisha wazi kuwa mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Zimbabwe anamwitaji zaidi kwenye kikosi chake.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema kuwa Ngoma bado ni mchezaji wa Yanga kwani mkataba wake unamalizika mwezi ujao na hivyo bado hajapata ofa kutoka timu yoyote ambayo inamwitaji.

“Ngoma amekwenda kutibiwa nyumbani kwao Zimbabwe, bado ana mkataba na Yanga hivyo naweza kusema ni mchezaji wetu, hatujapata ofa yoyote kutoka timu yoyote ambayo inataka kumsajili,” alisema Mkwasa.


Ngoma hajashuka dimbani kwa muda mrefu kutokana na majeruhi, huku taarifa nyingine zikidai anataka kuitosa Yanga.

No comments