ROBERTO PIRES AWABEMBELEZA OZIL, SANCHEZ KUBAKI EMIRATES

NYOTA wa zamani wa Arsenal, Roberto Pires ni kama kawaangukia mastaa wa klabu hiyo, Alexis Sanchez na Mesut Ozil, baada ya kuwataka wasiondoke na badala yake wasaini mikataba mingine na vinara hao wa Ligi Kuu England.

Sanchez, Ozil wanatarajiwa kuwa nje ya mikataba yao ifikapo Juni, mwakani jambo ambalo limezua tetesi kuhusu hatma yao.

Msimu uliopita Arsenal iliumaliza ikiwa nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi huku Sanchez akiwa ameifungia mabao 24 na kutoa pasi zilizozaa mengine 10 wakati Ozil akiwa amefunga nane na kusaidia kupatikana mengine tisa.

Kutokana na hali hiyo, Pires ambaye aliwahi kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu wakati akikipiga Gunners licha ya kumtaka kocha wa klabu hiyo, Arsene Wenger kutumia kiasi kikubwa ili kusuka kikosi hicho, anasema pia suala la kuwafunga kitanzi Sanchez na Ozil ni jambo la muhimu sana.

“Nina matumaini na niwaombe wasaini kataba mpya kwasababu wote wawili ni muhimu na ni wachezaji wanaonogesha kikosi,” alisema staa huyo wa zamani katika mahojiano yake na Sky Sports.

“Tunahitaji mashujaa kama Sanchez na tunamuhitaji Ozil,” aliongeza staa huyo wa zamani.


“Sifahamu kitakachotokea mwishoni mwa dirisha la usajili, lakini Wenger ana kazi kubwa ya kufanya majira haya ya joto,” Pires alikwenda mbali zaidi.

No comments