RONALDO AMTAJA ANDRE SILVA KAMA MWOKOZI MPYA WA SOKA LA URENO

WACHAMBUZI mbalimbali akiwemo pia mwanasoka bora wa dunia, Cristiano Ronaldo wamemtaja Andre Silva kama mwokozi mpya wa Ureno.

Ronaldo amemtabiria mazuri Andre Silva katika siku zijazo na akasisitiza kwamba hata yeye akiondoka anaamini Ureno itakuwa salama.


“Kama nikistaafu soka naamini bado Ureno itakuwa salama kwani tuna mshambuliaji bora Andre Silva ambaye anakuja juu na ana uwezo mkubwa sana,” alisema Ronaldo.

No comments