Habari

RONALDO APIGWA BAO KWA UINGIZAJI WA MKWANJA MREFU ULAYA

on

UNAWEZA kuitazama vipi hii?
Kwamba pamoja na ukweli kuwa mshambuliaji wa Real Madrid ya Hispania na timu ya
taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo pia ndie mwanamichezo anayeingiza fedha
nyingi zaidi duniani, lakini kuna watu wengine kiboko yake.
Jarida la Forbes limetoa orodha
ya watu maarufu 100 wanaoingiza fedha nyingi na nyota huyo wa Real Madrid na
Portugal anashika nafasi ya tano.
Ronaldo ameporomoka kwa nafasi
moja kutoka ya nne mwaka 2017 lakini mvaa jezi namba saba huyo anaingiza pauni
mil 73.2 kwa mwaka.
Pato la mshambuliaji huyo
lilipanda zaidi baada ya kusaini mkataba mpya Novemba, mwaka jana Real Madrid.
Mchezaji huyo mwenye umri wa
miaka 32 amesaini mkataba ambao analipwa pauni 365,000 kwa wiki uwanja wa
Santiago Bernabeu hadi mwaka 2021.
Mbali ya hiyo, Ronaldo ana
mkataba binafsi na Nike wenye thamani ya pauni mil 790 wakati kampuni yake ya
CR7 nayo inazidi kukua.
Ronaldo anatarajiwa kushinda
Ballon d’Or ya tano mwaka huubaada ya kuiongoza Real Madrid kutwaa taji la
kwanza la la Liga tangu mwaka 2012 pamoja na taji la Ligi ya Mabingwa kwa mara
ya pili mfululizo mapema mwezi huu.
LeBron James ni mwanamichezo
mwingine pekee ambaye yumo kwenye orodha hiyo pamoja na rapa Sean “Diddy” Combs
kwamba ndie mwenye mabunda mengi zaidi akiwa na utajiri wa pauni mil 102.
Msanii machachari, Beyonce
Knowles yeye amekuwa katika nafasi ya pili akisunda kitita cha pauni mil 82,
wakati JK Rowling anakamata nafasi ya tatu kwa kiasi cha pauni mil 74.8.
Mtukutu mwingine duniani, Drake
yeye amevuka malengo na kuwa na utajiri wa pauni mil 74.06 anazoingiza, wakati
Ronaldo ndiye anashika nafasi ya tano kwa kitita cha pauni mil 73.2.

Wanaofuatia ni The Weeknd akiwa
na pauni mil 72.45, Howard Stern akiwa na mabunda yanayofikia pauni mil 70.86,
Coldplay yeye akiwa na pauni mil 69.33, James Patterson pauni mil 68.53 na
mwisho katika kumi bora ni LeBron James pauni mil 67.8.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *