ROONEY SASA AAMUA KUSITISHA KUONDOKA UNITED

WAYNE Rooney ambaye ni nahodha wa Manchester United ameripotiwa kutaka kusitisha mpango wake wa kutaka kuondoka Old Trafford.

Nyota huyo ambaye amewahi kuchezea Everton alikuwa akiwindwa na timu za China, baada ya kukosa namba ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza.


Mshambuliaji huyo atafanya maamuzi ya mwisho atakaporejea kutoka mapumziko baada ya tetesi kuvuma kuwa huenda akarudi Everton au kutimkia China uhamisho wa majira ya joto.

No comments