STAA wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka amewatahadhalisha wanawake wenzake kwamba wasiwasamehe wanaume wanaowanyanyasa kimapenzi ndani ya nyumba zao, kwakuwa kufanya hivyo ni kujinyima haki zao kisheria.

Rose amesema, mwanamke anayejielewa hatakubali kunyayasika awapo kwenye ndoa yake na anayeogopa ni yule asiyejitambua bali anaishi ilimradi kaolewa.

“Huwa nachukizwa sana na mwanamke anayekubali kunyanyaswa katika ndoa na kujifanya mvumilivu, wakati karne hii mwanamke wa aina hiyo anadharaulika na jamii yote inayomzunguuka kwakuwa hatambui thamani yake,” amesema Ndauka.


Ameongeza kuwa, wanawake wanaofichua manyanyaso wanaofanyiwa na wenzi wao huwa mashujaa na umma hujifunza kupitia kwao, badala ya kuficha na kuugulia ndani kwa ndani huku ukiishia kuteketea moyoni au kujiua.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac