ROSS BARKLEY KUWAINGIZA VITANI WENGER NA MOURINHO


WAKATI Arsene Wenger akijifikiria kufungua pochi kukamilisha lengo lake la kumsainisha kiungo Ross Barkley wa Everton, Manchester United iko tayari kuweka mezani ofa ya pauni milioni 40 kwa ajili ya nyota huyo wa kimataifa wa England.

Barkley (23) amebakisha miezi 12 Goodison Park na kocha Ronald Koeman amesema atamtia sokoni kama atakataa kusaini nyongeza ya mkataba wake.


Arsenal imeonyesha nia ya kumsajili Barkley tangu miezi sita iliyopita na inamtazama kiungo huyo kama mbadala sahihi wa Mesut Ozil kama Mjerumani huyo atashinikiza kuondoka katika dirisha la usajili wa kiangazi.

No comments