SAID NDEMLA ACHAGUA KUBAKI MSIMBAZI... apotezea tetesi za kutua Jangwani

KIUNGO mshambuliaji Said Ndemla ameamua kubaki Simba baada ya kuelezwa kutaka kuhamia upande wa pili, ilielezwa hivi karibuni kuwa kiungo huyo yumo kwenye rada za wana Jangwani wakitaka kumsajili kama ilivyokuwa kwa Ibrahim Ajibu Migomba.

Akiongea na saluti5, Ndemla amesema haoni sababu ya yeye kujiunga na Yanga kwani ni timu ya kawaida inayofanana na Simba kwa kuwa na wingi wa mashabiki na amemtakia kila la kheri swahiba wake, Ajibu ambaye amejiunga na mabingwa hao wa bara.

Akizungumzia uvumi uliozagaa, Ndemla amesema hakuwahin kuzungumza na kiongozi yeyote wa Yanga isipokuwa nae alikuwa akisikia taarifa hizo kupitia mitandaoni, amesema hakuwa na mipango ya kutaka kwenda Yanga, hivyo, amawahakikishia wapenzi na mashabiki wa Simba kukaa mkao wa kula.

Said Ndemla, mmoja kati ya viungo wenye mashuti makali, ametajwa katika orodha ya wachezaji wanaotakiwa na Yanga ambayo iliwekwa mitandaoni na kauli hiyo imeondoa ubishi kuwa Ndemla anasalia Simba na wala haendi kokote.

Awali Ndemla alihitajiwa na timu ya Eskelstuna ya nchini Sweden lakini Simba walikataa kumruhusu wakiamini mchango wake katika kikosi hicho ni mkubwa sana, hata hivyo mchezaji huyo alizuiwa tena asiende Afrika Kusini ambako alitakiwa na klabu moja ya Ligi Kuu.


Samba sasa ina viungo wanne wa kushambulia ambao ni Muzamiru Yassin, Mohammed Ibrahim, Ndemla na Shiza Kichuya, bado usajili unaendelea na wakati wowote anaweza kuongezwa kiungo mwingine.

No comments