SALUM KIMENYA AONYESHA "SINTOFAHAMU" KUTOSWA KIKOSI CHA TAIFA STARS

BEKI wa timu ya Tanzania Prisons, Salum Kimenya ameshangazwa na kitendo cha kutojumuishwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa Stars ambayo inajiandaa kucheza dhidi ya timu ya Lesotho Jumamosi hii kwenye dimba la uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam majira ya saa mbili usiku.

Beki huyo ametuma ujumbe kwenye akaunti yake ya facebook akionyesha kushangazwa kuachwa kwenye mchezo huo baada ya kufanya vyema akiwa na klabu yake ya Tanzania Prisons.

“Pasipo MUNGU hakuna chochote naomba tu unipe nguvu zaidi kwakuwa Tanzania ndio nchi pekee yenye wachezaji maalum wa kucheza timu ya taifa kutoka kwenye klabu kubwa,” ilisomeka sehemu ya taarifa yake.

Salum Kimenya ameachwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa Misri kwa ajili ya maandalizi ya mechi dhidi ya Lesotho ambapo Hassan Kessy na Shomari kapombe ndio wameshikilia namba ya Kimenya kwenye timu ya taifa.

Salum Kimenya ameachwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichokuwa Misri kwa ajili ya maandalizi ya mechi dhidi ya Lesotho ambapo Hassan Kessy na Shomari kapombe ndio wameshikilia namba ya Kimenya kwenye timu ya taifa

No comments