SAMATTA ASEMA UDOGO WA UWANJA WA AZAM COMPLEX UMEWAKOSESHA USHINDI DHIDI YA LOSOTHO

MSHAMBULIAJI wa timu ya taifa “Taifa Stars”, Mbwana Samatta amesema kwamba udogo wa uwanja wa Azam Complex, Chamazi Dar es Salaam ndio uliowakosesha ushindi dhidi ya Lesotho Jumamosi iliyopita.

Mbwana ambaye anacheza soka la kulipwa Ubelgiji akiwa nahodha wa Stars aliongoza timu hiyo kupata sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi L kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.

Stras inayofundishwa na kocha Salum Mayanga, ilitangulia kwa bao la Samatta dakika ya 27 kwa shuti zuri la mpira wa adhabu ndogo kabla ya Lesotho kusawazisha kupitia kwa Thapelo Tale dakika ya 34.

Na baada ya mchezo, Samata akasema: “Uwanja wa Azam Complex ni mdogo sana kitu ambacho kwa upande wetu wengi tumezoea kucheza uwanja mkubwa wa taifa, imetufanya tujibane, tumeshindwa kucheza kwa uwezo wetu mechi ya leo, yaani ukipewa mpira ukigeuka uwanja umekwisha,” alisema.

Samatta pia akalaani staili ya ukabaji ya mabeki ya Lesotho akisema walikuwa wakimfuata watatu kwa wakati mmoja hadi kuna wakati akajikuta anakasirika.


Nimekasirishwa na kitendo cha kutoka sare na Lesotho, sijafurahishwa kabisa hasa ukiangalia tumecheza nyumbani na haikuwa akilini mwangu kama matokeo yangekuwa hivyo, lakini ndio imekuwa hivyo. Tunawaahidi Watanzania tutafanya vizuri katika mechi zijazo.”

No comments