SEYDON WA “SIO POA” AWAFICHA MAUA SAMA NA RUBY

YULE mkali wa bongofleva anayetamba sasa na kibao ‘Sio Poa’, Said Makamba ‘Seydon’ ametamba kuja na kazi ya ‘kilo’ ambayo ndani yake kutakuwa na sauti ya mmoja kati ya waimbaji Maua Sama au Ruby.

Akiongea kwa niaba ya Seydon, Produza wa Studio ya BM Records inayopika kazi hiyo, Mantano, amesema anaamini kwamba sasa anampika na kumuivisha Seydon mwingine kabisa kwenye muziki kupitia wimbo huo.

 Mantano ambaye Studio yake iko Kigogo Luhanga, jijini Dar es Salaam, amesema kazi tayari imeshakamilika kwa kila kitu na wanachosubiri sasa ni kukubaliana na mmoja kati ya wasanii Ruby na Maua Sama ili kumalizia kwa kuingiza sauti zao.

“Kibao kipo katika miondoko ya Zouk Rhumba ya kisasa kabisa ambapo Seydon ameonyesha ufundi wa hali ya juu kiuimbaji kiasi hata mimi mwenyewe amenishitua,” amesema Mantano ambaye ni kati ya maproduza wakali zaidi Bongo.

Kwa mujibu wa Seydon mwenyewe, hadi kufikia hatua ya kupika kazi hiyo ambayo anaamini itakapotoka itasumbua nchi nzima, ni watu wawili tu ndio wamehusika zaidi kutoa mchango mkubwa, ambao ni Mantano na mwingine aliyemtaja kwa jina la Hatibu Munga ‘Baba Warda’.


“Huyu Hatibu mdau wangu mkubwa sana anayeishi Msimbazi Centre, jijini Dar es Salaam na amekuwa akinisapoti karibu kila hatua ninayopiga, Mungu ambariki sana aisee,” amesema Seydon.

No comments