SHANIA KABEYA AWAKOGA "SHILAWADU" KATIKA KAZI YAKE MPYA YA MDUARA

KIBAO "Shilawadu" cha mkali mpya wa kike wa bongofleva, Shania Kabeya kimekamilika na kinatarajiwa kuachiwa rasmi wakati wowote kuanzia sasa, imefahamika.

Akiongea na saluti5, Shania amesema anaamini "Shilawadu" kilichorekodiwa ndani ya Studio za ‘442 Records’ zilizo chini ya mtayarishaji Mubanga na ambacho kipo katika miondoko ya mduara, kitawashika mashabiki wengi kutokana na meseji yake kuwa kali.

Amesema kuwa, katika wimbo huo amevaa uhusika wa mtu anayemsihi mpenzi wake kuangalia mustakabali wa mahaba yao na kutoyasikiliza maneno ya watu wa pembeni aliowaita kwa jina la ‘Shilawadu’.

“Hivi sasa niko kwenye mchakato wa kupanga siku rasmi ya kukiachia kibao hicho ambapo nitakisambaza kwenye vituo mbalimbali vya radio hapa Bongo pamoja na mitandao ya kijamii kwa ajili ya utambulisho kwa mashabiki,” amesema Shania.


Kabla ya wimbo huo wa "Shilawadu", Shania ambaye nje ya muziki ni mfanyabiashara wa vipodozi, hivi karibuni alipakua kazi yake ya kwanza inayokwenda kwa jina la ‘Penda Unapopendwa’ iliyoko kwenye miondoko ya mchiriku wa kisasa.

No comments