SHANIA KABEYA AZIDI KUTIKISA NA “SHILAWADU” YAKE

KILE kibao cha mduara kinachokwenda kwa jina la ‘Shilawadu’ kilichoimbw na msanii Shania Kabeya, kimeonekana kuzidi kushika chati na kuwateka mashabiki wengi zaidi wa muziki Bongo.

Kibao hicho ambacho ni cha pili kwa Shania, kimeachiwa rasmi takriban wiki mbili zilizopita, lakini kimetokea kuwa gumzo kubwa jijini Dar es Salaam pamoja na mikoa mingine yote ya Tanzania.

Mashabiki mbalimbali walioongea na ripota wetu wamekiri kupagawishwa na kibao hicho, hasa kutokana na ujumbe wake kuwa ni unaokwenda na wakati tulionao sasa na midundo pia kuwa ni ile inayochezeka zaidi.

“Binafsi, nimekuwa napendelea mara kwa mara kusikiliza kibao hicho ninapokuwa nyumbani, kwasababu kinaniliwaza maana ‘mashilawadu’ wapo kibao mtaani kwetu wanaotufuatilia mimi na mpenzi wangu,” amesema shabiki mmoja aliyejitaja kwa jina la mama Hafidhi.


Kwa sasa kibao hicho cha msanii huyo ambaye nje ya sanaa ni mfanyabiashara wa vipodozi, kimemwagika kwenye vituo mbalimbali vya radio pamoja na mitandao yote ya kijamii.

No comments