SHETTA ASEMA HAONI FAIDA YA KUWA NA "TEAM" KATIKA MUZIKI

MWIMBAJI wa muziki wa kizazi kipya, Shetta amesema kuwa hana timu ya kimuziki kama ilivyo kwa Diamond Platnumz na Ali Kiba ambao kila kukicha huongeza idadi ya watu katika timu zao.

Shetta amesema kuwa hatambui uwepo wa timu hizo kwa sababu haoni tija yake kwenye kazi zake za sanaa.

“Sina timu na wala siamini kama kuna kitu kinaitwa timu kati ya Diamond na Kiba, mimi si aina ya watu wanaoamini kufanya muziki kwa mtindo wa timu,” alisema rapa huyo.
“Sioni kama zina msaada sana kwenye sanaa au zinaweza kumbeba msanii,” aliongeza.


Kumekuwa na timu mbili kubwa za kimuziki hapa Bongo ambazo zimewagawa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kati ya Diamond na Kiba.

No comments