SIKIA HII... ETI PATCHO MWAMBA AMEWAMISS MASHABIKI WANAORUSHA PESA JUKWAANI WAKATI WANATUMBUIZA!

STAA wa muziki wa dansi, Patcho Mwamba ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa siku hizi mashabiki wamekuwa hawarushi tena fedha jukwaani kwasababu ya ukata wa kimaisha.

Patcho ambaye pia ni mcheza filamumaarufu, alidai kuwa suala la uhaba wa fedha linaloendelea nchini limesababisha mashabiki kushindwa kuwatuza wanapokuwa jukwaani wanapotoa burudani.

“Pesa imekuwa ngumu kidogo, siku hizi hakuna msanii anayetuzwa jukwaani kama zamani, watu wako bize na masuala ya msingi tu,” alisema Patcho.


Staa huyo mwenye asili ya Congo (DRC), amekuwa akifanya kazi zake nyingi na JB, huku kivutio kikubwa kwa mashabiki kikiwa ni lafidhi yake ya Kikongo.

No comments